Kwa ufupi:
Nishati ya miti (mkaa na kuni) ni aina ya nishati inayotumika zaidi kwenye kupikia na
kwenye kuota moto kusini mwa Jangwa la Sahara na hutumika kwenye biashara ndogo
ndogo kama migahawa, uokaji, biashara za mamantilie, utengenezaji wa matofali, pamoja
na ukaushaji wa mazao kama chai na tumbaku.
Zaidi ya 90% ya wakazi kusini mwa Jangwa la Sahara inategemea ama kuni au mkaa.
Nishati ya miti huchangia yapata 90% ya nishati ya miti nchini Tanzania.
Mkaa unatumika zaidi mijini wakati kuni hutumika zaidi vijijini. Yapata 70% ya kaya za
mijini hutegemea mkaa.
Afrika huzalisha 62% ya mkaa wote duniani ambao unakisiwa kufikia tani milioni 52.
Tanzania inashika nafasi ya saba kwa uzalishaji wa mkaa duniani, ikichangia kama 3% ya
uzalishaji wa mkaa wote duniani, kwa kiasi cha zaidi ya tani 1.6.