Kwa ufupi:
Japokuwa kitengo cha Kilimo Hifadhi (CFU) hakihimizi matumizi ya Viua Magugu vya aina fulani au
Viuatilifu vingine vya kukinga mimea, wakulima wanafahamu kuwa Viua Magugu vikitumika kwa
usahihi aidhaa kwenye Kilimo Hifadhi au Kilimo cha mazoea huokoa muda mwingi unaotumika
kwenye palizi linaloumiza mgongo. Wakulima ambao wanatumia viuatilifu hivi kwa usahihi wanaokoa
muda mwingi na gharama zinazotumika kuajiri vibarua kufanya palizi. Wazalishaji na wafanyabiashara
wanaosambaza Viua Magugu na Viuatilifu vingine vya mimea wamerahisisha upatikanaji wa viuatilifu
husika kote nchi Zambia na ukanda mzima wa kusini mwa Afrika. Hii imefanya wakulima wengi
kununua na kutumia viuatilifu mara kwa mara kwenye mashamba yao bila hata kuwa na
mafunzo/elimu yakutosha.
Wakulima aidha wa Kilimo Hifadhi au wa kilimo cha mazoea hutumia viuatilifu katika mfumo wao wa
uzalishaji ili kuongeza kipato kwa lengo la kuongeza ubora wa maisha katika familia. CFU ni shirika
kubwa na lenye uzoefu wa kutoa mafunzo ya Kilimo Hifadhi nchini Zambia na kwingineko. Hivyo basi,
itakuwa ni kutokuwajibika kama CFU haitatoa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.
CFU inaendelea kutoa mafunzo ya kina kuhusu Viua Magugu na matumizi yake kwa
wafanyakazi/watumishi wake wote. Mafunzo haya hutolewa kwa Mabwana shamba ambao nao
wanawafundisha waratibu wa wakulima. Baada ya hapo waratibu hutoa mafunzo hayo kwa wakulima
wengine. Mafunzo haya ni kwa yeyote anayetaka kushiriki na hakuna malipo au gharama yoyote.
Watumishi wengi kutoka wizara ya kilimo na kutoka mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali
wamenufaika na mafunzo haya yanayotolewa kwa kina na kwa mbinu shirikishi.
Kijitabu hiki kimeandaliwa na CFU kama muhtasari wa mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viua
Magugu ambayo yameshatolewa kwa maelfu ya wakulima na wanyunyizaji wa viatilifu hivi. Kijitabu
hiki hakilengi kuwa mbadala wa mafunzo ya ana kwa ana.