Kwa ufupi:
Mkulima anatakiwa kutafuta soko la mazao yake kabla hajaanza
shughuli ya uzalishaji shambani. Ili kupata taarifa za kutosha,
mkulima anashauriwa kufanya utafiti wa soko. Mkulima anaweza
tumia njia kuu mbili: (i) kuandaa dodoso na kuwauliza wadau
muhimu wa soko la zao alilozalisha na, (ii) kutembelea masoko ya
mazao na kukusanya taarifa kwa njia ya kuona. Utafiti wa soko
humwezesha mkulima kutoa maamuzi sahihi juu ya uuzaji wa
mazao yake. Katika kuuza mazao, mkulima lazima azingatie
sheria, kanuni na taratibu za nchi na soko husika. Pia, ni muhimu
kuelewa namna nguvu ya soko inavyofanya kazi. Hii itamsaidia
mkulima kujua lini ayapeleke mazao sokoni na hivyo kupata bei
nzuri zaidi