Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya
Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Norway (NLH),
kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la
Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao
ulianza rasmi mwezi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali
ya Norway. .
Chapisho hili Iinawasilisha mwenendo wa Warsha ya saba ya
Wakulima wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhusu Athari za
Uharibifu wa Mazingira katika Uhakika wa Chakula na Pato la
Kaya iliyofanyika Kituo cha Jeshi la Wokovu, Kurasini, Dar es
Salaam, 2-4 Desemba 2003. Mwenendo wa warsha
umechapishwa na kutolewa katika lugha ya Kiswahili na
Kiingereza.
Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya
mradi na kuimarisha uhusiano kati ya wakulima, watafiti na
wataalamu wa ugani ni kufanya warsha zenye madhumuni
yafuatayo:
1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na wataalamu wa
ugani ili kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji
kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha
kilimo na ufugaji
2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili
wakulima wadogowadogo
3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au
kipaumbele
4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya
kilimo na mifugo.