Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) pamoja na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Norway (NLH) wakishirikiana na Wizara ya Kilimo na
Chakula (MAFS), wamekuwa wakitekeleza mradi wa "Uhakika Wa
Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogowadogo" (TARP II -
SUA Project). Mradi ulianza mwaka 2000 na unagharamiwa na Serikali
ya Norway pamoja na serikali ya Tanzania.
Madhumuni ya warsha hii yanalenga kuleta ushirikiano wa karibu kati ya
wakulima wadogo wadogo ngazi ya kaya, wagani, wawakilishi wa
mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na watafiti wa kilimo na mipango
katika kuinua uwezo wa maisha ya mtanzania katika ngazi ya kaya;
kiuchumi, kiafya na maendeleo kwa ujumla. UKIMWI ni tatizo kubwa
linatishia kuwepo kwa binadamu. UKIMWI hauishii kumuua muathirika
na kupoteza nguvu kazi tu, lakini pia jamii ya muathirika huathirika kwa
narnna moja au nyingine. Nguvu kazi ya muathirika hupotea kwa ajili ya
kumuuguza mgonjwa; fedha nyingi hutumika kwani mgojwa anahitaji
chakula maalum na dawa; watoto hukosa huduma ya wazazi na hivyo
kushindwa kusoma au kupata lishe bora; mgonjwa anapofariki kuna
gharama za mazishi na nguvu kazi-hupotea kuhudumia misiba. Warsha
ililenga kubaini mtazamo wa jamii kuhusu athari za UKIMWI katika
uhakika wa chakula na kukuza elimu ya UKIMWI na lishe bora kwa
kutumia wataalamu walioshiriki.