Kwa ufupi:
Shughuli za utafiti chini ya Programu ya Mageuzi ya Kilimo na
Maliasili kwa Maisha Bora (PANTIL) zilianza rasmi mwanzoni mwa
mwezi Januari 2006. Lengo la programu hii ambayo itatekelezwa
kwa muda wa miaka minne (2005-2009) ni kuchangia ukuaji wa
uchumi, kupunguza umaskini na kuboresha ustawi wa jamii kwa njia
ya uboreshaji wa sekta za kilimo na mali asili. Programu hii inazo
sehemu kuu mbili. Sehemu ya kwanza inashughulikia utafiti na
uwezeshaji wa wakulima; na sehemu ya pili inashughulikia mageuzi
ya kitaasisi na kuboresha uwezo wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) ili kiweze kutekeleza majukumu yake ya kitaaluma.
Shughuli za uwezeshaji wa wakulima zina lengo la kuwaongezea
uwezo wakulima ili waweze kudai elimu husika, teknolojia inayofaa,
pamoja na habari ill kuboresha tija, faida na kuchangia katika
kuongeza kipato na kupunguza umaskini. Baadhi ya shughuli
kadhaa ambazo zitafanyika katika kipindi cha 2006 hadi 2009 ni
kama zifuatazo:
• Uimarishaji wa vyama/vikundi vilivyopo vya wakulima na
uanzishaji wa vikundi vipya kupitia mafunzo ambayo yatahusu
uanzishaji vikundi, uendeshaji wake, na uongozi. Shughuli hizi
zitahusisha uongozi husika, wadau katika ugani zikiwemo asasi
zinazofundisha maafisa ugani.
• Kusaidia kuanzisha shule za wakulima katika vijiji na wilaya
zitakazochaguliwa
• Uchapishaji na usambazaji wa nyenzo za ugani kama vile
vipeperushi, vijitabu, n.k.
• Uimarishaji wa mbinu za wakulima ili waweze kushiriki katika
kutoa mafunzo na usambazaji wa teknolojia mpya kwa wakulima
wengine, na kuyafikia maeneo yaliyo nje ya programu ili yaweze
kufaidika na programu