Kwa ufupi:
Mboga za kiasili ni muhimu kwa chakula na zina virutubishi zaidi ya zile za kigeni kama vile sukuma wiki na kabeji. Mifano yake ni kama vile sageti, mnavu, mchicha na mkunde. Mimea hii huwa na madini na vitamini A zinazohitajika kwa afya ya binadamu.