xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple
dc.contributor.author | Idara ya misitu na nyuki | |
dc.date.accessioned | 2024-09-02T10:08:34Z | |
dc.date.available | 2024-09-02T10:08:34Z | |
dc.date.issued | 2021-01 | |
dc.identifier.uri | http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/905 | |
dc.description | Jarida | en_US |
dc.description.abstract | Ufugaji Nyuki ni miongoni mwa sekta muhimu za kiuchumi nchini Tanzania, yenye mchango mkubwa kwenye maisha ya watu wengi mijini na vijijini. Sekta hii inakadiriwa kuajiri zaidi ya watu milioni mbili nchini kwenye mnyororo wake mzima wa thamani. Mazao ya nyuki kama vile asali, nta, chavua, gundi ya nyuki, maziwa ya nyuki na sumu ya nyuki, yanatumika yakiwa kwenye hali tofauti pia kama malighafi ya viwanda vya chakula, urembo, dawa, nguo, ngozi, umeme na mishumaa. Ufugaji Nyuki umedhihirisha kuchangia ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa kuongeza ubora wa mbegu na uhifadhi wa bioanuai kwa njia ya uchavushaji unaofanywa na nyuki. Kutokana na umuhimu kwenye uchavushaji, ufugaji nyuki umetambuliwa kama nyenzo ya uhifadhi. Pamoja na michango hii yote, bado sekta ya ufugaji nyuki haijaonekana kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na uzalishaji wa mazao ya nyuki kutokana na kutofuatwa kwa taratibu bora za ufugaji nyuki. Tangu kuanza kutumika kwa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, ambayo inahimiza uanzishwaji na umiliki wa Hifadhi za Nyuki na manzuki ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki, kumekuwa na maendeleo yasiyolingana kwenye maeneo tofautitofauti ndani ya sekta. Mfano, hakuna maendeleo yanayoridhisha kwenye uanzishwaji wa Hifadhi za Nyuki na manzuki. Aidha, kuna zaidi ya misitu 100 inayomilikiwa na Serikali na Sekta Binafsi iliyobainishwa kuwa hifadhi za nyuki lakini haijatangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya Ufugaji Nyuki Na. 15 ya mwaka 2002. Hali hii inaifanya baadhi ya misitu kupoteza hadhi yake ya kutumika kama hifadhi za nyuki na kutangazwa kisheria. Kwa miaka kadhaa, wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Serikali, Asasi Zisizo za Serikali (AZISE), Asasi za Kijamii, Sekta binafsi na vijiji vimeanzisha hatua za kutangaza Hifadhi za Nyuki lakini vimeshindwa kukamilisha hatua za kutangaza hifadhi hizo kisheria. i Sababu zilizokwamisha zinaweza kuwa ni pamoja na kukosekana kwa mwongozo unaoongoza na kusimamia uanzishwaji na usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na manzuki. Hivyo ili kuhakikisha utendaji wenye ufanisi na kiwango katika maeneo yote ya Hifadhi za Nyuki na manzuki; Wizara imeandaa mwongozo huu ili kuwaongoza wadau katika uanzishwaji na usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na Manzuki. Mwongozo huu, unalenga kutoa mwanga kwa wadau kuhusu taratibu za uanzishwaji na usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na manzuki pamoja na viwango vyake vya usimamizi wa uwandani. Serikali inatarajia kuwa mwongozo huu utakuwa nyenzo muhimu na ya msaada ya kuimarisha usimamizi na uanzishwaji wa Hifadhi za Nyuki na manzuki. Aidha, mwongozo huu utaimarisha uhifadhi wa rasilimali za nyuki na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa maendeleo endelevu. | en_US |
dc.description.sponsorship | Programu ya Mnyororo wa Kuongeza Thamani ya Mazao ya Misitu (FORVAC) | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania | en_US |
dc.subject | Mwongozo | en_US |
dc.subject | Usimamizi | en_US |
dc.subject | Uhifadhi wa nyuki | en_US |
dc.subject | Manzuki | en_US |
dc.title | Mwongozo wa uanzishwaji na usimamizi wa hifadhi za nyuki na manzuki Tanzania | en_US |
dc.type | Article | en_US |