Kwa ufupi:
Mkonge au Katani ni moja kati ya zao la biashara Jina la kisanyansi inaitwa Agave sisalana. Asili ya zao hili ni Mexico na baadae likasambaa katika nchi nyingine, kwa mara ya kwanza lilitambushwa katika nchi za kitropikia na subtropikia India,Tanzania, Brazil, Kenya south Africa, Angola, Mozambique Morocco Uganda, Zimbabwe na Mauritius.
Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka Pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan na kuisafisha kwa kupitia Frolida, Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo Kikokwe huko Pangani Tanga.
Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanganyika mpaka kufikia mwanzoni mwa miaka 1960 Tanganyika ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na mexico kwa mauzo ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi. Kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miaka ya 1970 uzalishaji ulipungua toka tani 230,000 hadi tani 19,700 kwa mwaka 1997.
Hata ivyo mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 ambayo yalilenga katika ubinafisishaji na biashara huria , uhuru wa taasisi za kifedha za ndani na nje ya nchi yalifufua kilimo cha mkonge na hasa kukamilika kwa ubinafishaji mwaka 2005 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40,000 mwaka 2015 hii inatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mkonge na bidhaa zake pamoja na kupanda bei kwenye soko la dunia pamoja na ndani.
Soko kuu la mkonge wa Tanzania ni china, Saudi Arabia , India, Uhispania, Ujerumani, Uingereza, Kenya, Uganda na Nigeria.