Kwa ufupi:
Katika Nyanda za Juu za Kusini ni Mikoa miwili tu (Iringa na Mbeya) ambayo idadi ya ng'ombe wa maziwa imeongezeka sang. Hii ni baada ya kuanzishwa kwa mradi wa kushughulikia wafugaji wadogo wadogo kati ya nchi ya Uswisi na Tanzania. Katika sehemu hizi nyasi za asili zilizopo ni zile za kuezekea na utafiti uliofanyika Uyole unaonyesha kuwa nyasi hizi kutoa chakula kidogo kwa msimu. Vile vile baada ya msimu wa-mvua kuanza nyasi hizi hukua upesi upesi na baada ya miezi miwili tu, hutoa mbegu na hivyo ubora wake kupungua. Hi mifugo ya kisasa iweze kutoa maziwa mengi inahitaji chakula chenye asili mia
protini zaidi ya saba kiasi ambacho hakipatikani kwenye nyasi za asili. Hivyo kwa ufugaji wa kisasa ni lazima mbinu nyingine za kuweza kupata malisho bora zitumike. Hata hivyo katika nyanda hizi msimu wa ukuaji wa mimea ni siku 180 tu yaani toka mwanzo wa Desemba hadi mwisho wa Mei. Baada ya hapo malisho hayakui kwa sababu ya baridi kali ya usiku, hasa mwezi wa sita mpaka wa nane, na baada ya hapo kwa ajili ya ukosefu wa unyevu. Hivyo tunakabiliwa na miezi sita ambayo lazima mbinu ya kupata chakula bora zitumike.