Kwa ufupi:
Kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kuzinduliwa kwa Tume ya Kitaifa ya Ardhi Februari 2013, hatua nyingi zimepigwa za kuboresha usimamizi wa ardhi nchini Kenya. Kuchapisha kitabu hiki ni ufanisi unaohitaji kusherehekea kwa sheria na kanuni mbalimbali ilizobuniwa katika kuzindua katiba ya Kenya inayolenga marekebisho katika sekta ya ardhi ambayo yamewekwa kukidhi mahitaji ya usawa wa jinsia katika masuala ya ardhi. Katiba mpya ndiyo kilele cha ongezeko la hatua zilizopigwa na nchi ili kuinua hadhi ya wanawake na maslahi yao katika ardhi. Katiba mpya inawakilisha hatua kubwa zilizopigwa kuboresha hadhi za wanaume na wanawake katika nyanja zote za maisha. Kwa sababu hiyo pana haja ya kuzingatia ufafanuzi wa ardhi kwa upana (maji na nafasi iliyopo) kama rasilimali
asilia na mali nyingine inayopatikana katika ardhi. Ardhi na mali nyingine (kama mifugo, madini yanayochimbuliwa, mashine na kadhalika.) inaweza kutumika kwa kilimo na uzalishaji na vile vile inaweza kuwa chanzo cha uwezeshwaji wa kisiasa miongoni mwa wanawake. Kuwa na uwezo wa kupata ardhi na mali kunatoa nafasi ya makazi na kuwawezesha wanawake kujiunga katika ushindani wa siasa kuhusu rasiliamali; ardhi ni mali inayostahili kujumuishwa katika ndoa na inaweza kutumika kama chombo cha kupata mikopo.