Kwa ufupi:
Mbaazi za mda mfupi hukomaa kati ya siku 120 hadi125 katika maeneo ya Morogoro,Tanga, Pwani, Mtwara na Dar es salaam.Katika ukanda wa juu kwenye baridi mbaazi za mda mfupi hukomaa kwa mda mrefu zaidi ya siku 120.Mbaazi za asili hukomaa kati ya siku 210 hadi 270.Mbaazi za mda mfupi hutoa mavuno mengi zaidi ya zile za asili iwapo zitalimwa kwa kuzingatia maelezo ya kitaalamu.