Kwa ufupi:
Kijitabu hiki kinatoa matokeo ya mradi wa miaka 4 (2011-2015) yaliyofanywa na wanajiografia wanne kutoka chuo kikuu cha Stockholm. Utafiti huu ulifanyika katika vijiji vidogo viwili, ambavyo ni Siipow nchini Kenya na Engaruka nchiniTanzania. Kwa ujumla mradi huu uliangalia vitu vikuu vitatu: udongo, hali ya hewa na nguvu kazi. Mambo haya makuu yanaweza kuonyesha aina ya mabadiliko yaliyowahi kujitokeza katika mifumo ya umwagiliaji katika maeneo haya na sababu mahususi zilizosababisha mabadiliko hayo. Katika kijitabu hiki matokeo ya utafiti yameonyeshwa kufuatana na maeneo ya utafiti na hususani: mbinu za kilimo, mgawanyo wa majukumu ya kazi kwa wanawake na wanaume, sifa za udongo na maji, mabadiliko ya hali ya hewa na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na jinsi ambavyo mambo haya yote kwa ujumla yamekuwa yakibadilika kadri muda unavyokwenda.