Kwa ufupi:
Ukulima wa maharagwe, kunde, karanga na maharagwe soya una faida
nyingi kama vile kuweka naitrojeni kutoka hewani na kuboresha rutuba ya
udongo.
Ø Nafaka za jamii kunde zina protini kiwango cha juu na zaweza
kutayarishwa ili kupata vyakula vyenye virutubisho zinazosaidia
kukamilisha vyakula vya aina ingine.
Ø Mchanganyiko wa nafaka kuu (k.v. mchele, mtama, mbaazi na mahindi) na
jamii kunde ziwe kwa uwiano wa 70:30 ili kufikia kiwango kinachohitajika
cha amino asidi.
Ø Sifa na jinsi ya kutayarisha na kupika nafaka za jamii kunde nne muhimu
wakati zinapopikwa zimeelezwa. Muhimu pia kwa mapishi ya nafaka hizi
ni uzito na ujazo (ml) hivyo elimu kuhusu zana za vipimo imetolewa kwa
njia rahisi ya kutumia vikombe na vijiko vya kawaida.
Ø Kijitabu hiki kinasaidia watu wa mashinani Afrika kuboresha ufahamu wa
kuandaa chakula cha nafaka za jamii kunde.
Ø Kimetoa elimu ya utunzaji na maandalizi ya nafaka baada ya kuvuna, jinsi
ya kulinda ubora wa nafaka ili kufikia viwango vilivyowekwa na viwanda
hivyo kuongeza faida ya mazao na kusababisha nguvu kiuchumi na ustawi
vijijini.
Ø Vyombo muhimu na jinsi ya kuzitumia ili kuhakikisha ubora wa nafaka za
jamii kunde baada ya kuvunwa na kabla zipelekwe sokoni pia zimeelezwa
kwa kina.
Ø Aidha kuna habari juu ya utungaji wa lishe ya jamii kunde hizi, jinsi ya
kuzisindika ili kutoa mapishi ya thamani bora kutumia mbinu kadhaa na
rahisi kutayarisha pamoja na taratibu na sheria za ugombea upishi.