Kwa ufupi:
Mfumo wa Stakabadhi za Maghala ni mfumo unaotumika nchini wa kutumia bidhaa
zilizohifadhiwa kwenye maghala badala ya mali zisizohamishika kuwa dhamana ya
kupata mikopo kutoka asasi za fedha. Mfumo kama huu pia unatekelezwa nchi nyingine
za bara la Afrika pamoja na mabara ya Ulaya na Amerika.
Kwa kufuata mfumo huu wakulima wadogo na wakati wakiwa kwenye Ushirika au
Vikundi vya wakulima wanakuwa na nguvu ya soko na kuingia katika soko la ushindani
ambalo ingekuwa vigumu kutokana na kukosekana kwa mitaji. Pia mfumo huu unasaidia
kuzuia upotevu wa mazao unaotokana na uhifadhi dhaifu, kuhifadhi mazao ili kusubiri
kuuza wakati muafaka na pia kuongezea bidhaaa thamani kabla ya kuziuza.