Kwa ufupi:
Rutuba ya ugongoimefafanuliawa kama “uwezo wa udongo kusambaza idadi ya kutosha ya
virutubisho muhimu na maji yanayohitajika kwa ajili ya ukuaji wa mimea maalum
ikiongozwa na vigezo vya kemikali, maumbile, kibaiologia kwenye udongo.”
Kilimo ni chanzo kikuu cha chakula na kipato kwa idadi kubwa ya wakazi wa nchi zilizopo
kusini mwa jangwa la Sahara. Udongo ambao hauna rutuba nzuri ni kikwazo kikuu cha
kuongeza uzalishaji wa chakula, lishe na vyakula vya nyuzi nyuzi. Kuna uhaba wa matumizi
ya pembejeo za kilimo kusini mwa jangwa la Sahara. Ongezeko wa watu unasababisha
kupungua kwa ukubwa wa ardhi, na kwa kuwa kuna upungufu wa ardhi yenye rutuba kuna
umuhimu wa kufuata taratibu za sayansi ya udongo na uzalishaji mazao.