Kwa ufupi:
Kujifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu kwa wakulima kwa sababu ya athari
wanayoweza kuwa nayo kwenye kilimo. Wakulima wanaweza kutarajia kiasi cha joto kilichopanda
na dhoruba za mara kwa mara, mafuriko na hali za ukame. Hali ya hewa itakuwa
inabadilikabadilika zaidi na hivyo ngumu kutabiri. Wakulima wanahitaji kuelewa mabadiliko ya
hali ya hewa na anga ili kufanya mipango kuhusu mavuno yanayobadilika na tofauti, ukosefu wa
maji, na uwezekano wa ongezeko la wadudu waharibifu na magonjwa.
Makala haya yanatoa habari msingi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa itakayokusaidia kutayarisha
vipindi vya redio kuhusu mada hii. Unavweza kuwaambia wakulima katika eneo lako kuhusu njia
kadhaa ambazo kwazo, mabadiliko ya hewa huwaathiri wakulima. Kisha unaweza kujadili
mikakati ambayo wakulima wa eneo hilo wanaweza kutumia ili kufanikiwa katika kukabiliana na
mabadiliko ya hali ya hewa. Ongea na wakulima ili uelewe changamoto yao imekuwa nini
kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa. Je, wamepata njia mpya, au kutumia njia za jadi
zinazowasaidia kukabiliana na hali hii mpya.