Kwa ufupi:
Leo tunakwenda kujifunza kuhusu Udongo, aina za udongo, virutubisho vilivyopo kwenye udongo
pamoja na upimaji wa udongo.
Udongo ni nini?
Udongo ni tabaka juu ya ardhi ambalo hufanya kazi kama chombo cha kukuzia mimea.
Udongo hujengwa kutokana na shughuli zinazoendelea za hali ya hewa kulingana na vipengele
kadhaa vya mazingira. Kwa sehemu kubwa kuundwa kwa udongo hutawaliwa na vipengele
vikuu vitano: hali ya nchi (k.m. mvua, joto na upepo), mwinuko wa eneo (mahali eneo lilipo),
viumbe hai (mimea na vijidudu), asili ya kitu kilichozalisha udongo (aina ya miamba na madini
ambayo udongo unatokananayo) na muda.