Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na
Wizara ya Kilimo na Chakula (MAFS), pamoja na Chuo Kikuu cha
Kilimo cha Norway (NLH), kinatekeleza Mradi wa Uhakika wa
Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo wadogo Tanzania.
Lengo mojawapo katika mradi huu ni kuimarisha uhusiano kati ya
Wakulima, Watafiti na Washauri wa Ugani. IIi kufikia lengo hili,
mradi umepanga utaratibu wa kuwawezesha wakulima kutembeleana
ndani ya kanda zao na kati ya kanda na kanda.
Makala hii inawasilisha ripoti ya ziara iliyofanyika mwezi Agosti
2003. Ziara hii iliwashirikisha wakulima, wagani na watafiti kutoka
Kanda ya Mashariki na kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikijumuisha
Manispaa ya Morogoro, wilaya za lringa na Mbarali. Wanaziara
hawa waliwatembelea wakulima wa wilaya za Mbozi na Njombe ili
kuona na kujifunza zaidi kuhusu teknolojia muhimu ambazo tayari
wameazimia kuzitekeleza mara watakaporudi nyumbani kwao.
Taarifa hii pia inapatikana katika lugha ya Kiingereza.