Kwa ufupi:
Muhogo ni moja ya mazao ya mizizi hapa Tanzania
na nchi nyinqi za Africa. Muhogo una wanga
mwingi. Zao hili hustahimili ukame na hivyo
husaidia sana katika harakati za kupambana na
njaa hasawakati wa ukame.
Pamoja na umhimu wake, muhogo huharibika
upesi sana. Mara baada ya kuvunwa muhogo
huweza kuharibika ndani ya siku tatu au nne na
kutofaa kwa matumizi ya binadamu. Pia
usafirishaji wa muhogo kutoka sehemu moja hadi
nyingine ni mgumu na wa gharama kubwa. Hii
inatokana na mihogo kuwa na kiasi kikubwa cha
maji. Mambo haya husababisha hasara kubwa
kwa mkulima.