Kwa ufupi:
Mojawapo ya kikwazo kikubwa kinachomkwamisha mkulima mdogo kulima kwa tija
ni kumudu gharama za matumizi ya pembejeo za kilimo (mbolea na mbegu bora).
Katika kuhakikisha Serikali ya Tanzania inamsaidia mkulima kumudu gharama hizo,
mwaka 2008/2009 Serikali ilianzisha na kutekeleza utaratibu wa kuwapatia wakulima
pembejeo za kilimo kwa njia ya ruzuku kwa kupitia mfumo wa vocha (National Agricultural
Inputs Voucher System - NAIVS). Katika kufuatilia ufanisi wa mpango huu, utafiti umefanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), chini ya mradi
wa Enhancing Pro-poor Innovation in Natural Resources and Agricultural Value
Chains (EPINAV).