Kwa ufupi:
Kijitabu hiki ni matokeo ya mradi wa mwongozo wa mafunzo ya
Kilimo-hai Afrika na kilibuniwa kama kabrasha ya kuwagawia wakulima. Kama mkulima bila shaka unategemea mvua kupanda mazao yako na kufuga. Hata hivyo mvua zinaendelea kuwa haziaminiki na kusababisha mavuno kupungua au kukosekana kabisa. Mvua kubwa zinaweza kusomba udongo na kupunguza uzalishaji Ili kupunguza uhaba wa maji na kupotea kwa rutuba ya udongo, wakulima wa kilimo-hai huweka msisitizo katika uhifadhi wa udongo na maji.