Kwa ufupi:
NYUKI NI NINI? Nyuki ni wadudu wadogo wenye uwezo wa kuruka na hutengeneza vyakula vyao wenyewe kutokana na maji matamu yanayopatikana kwenye maua ya miti na ungaunga unaopatikana katika maua. Wadudu hawa wanauwezo wa kuziba matundu yanayojitokeza kwenye viota vyao kwa kutumia utomvu wa miti. Wadudu hawa ni wasafi sana hawapendi kuishi mahali palipo na harufu ya uozo wa kitu, ukungu, au maji maji (unyevu nyevu).