Kwa ufupi:
Utafiti huu wa athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa uchumi Zanzibar umetoa tathmini ya
athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi kwa visiwa hivi,njia muhimu za kuweza kukabiliana
nazo na fursa ya kupunguza ongezeko la hewa mkaa.Utafiti huu umegundua matokeo muhimu
yanayofafanuliwa kama ifuatavyo hapa chini.
Uchumi wa Zanzibar unategemea sana tabianchi na sehemu kubwa ya Pato la Taifa, ajira na
maisha yanahusiana na shughuli zinazotokana na tabianchi (za pwani, kilimo na utalii).
Tabianchi ya Zanzibar imebadilika katika miongo ya hivi karibuni.Tumeshuhudia ongezeko la
joto, mvua zisizotabirika,upepo mkali na bahari kupanda juu.Aidha, pia kuna ongezeko la
matukio mengi makubwa ( tafauti ya tabianchi).Jambo hili la mwisho limesababisha ukame na
mafuriko ambayo yameleta gharama kubwa za kiuchumi kwa Pato la Taifa. Matukio ya namna
hii yanaonekana kuongezeka. Aidha, ni wazi kuwa Zanzibar bado haijaweza kukabiliana ipasvyo
na tabianchi iliopo na kuna haja ya kuchukuwa hatua za haraka ambazo zinaweza kuleta faida
kubwa za kiuchumi katika kushughulikia kasoro za kukabiliana na hali iliopo.