Kwa ufupi:
Wakulima wengi Tanzania wanapata hasara kubwa inayosababishwa na
wadudu waharibifu wa mazao yanapohifadhiwa kwenye maghala. Uharibifu
huu unatishia uhakika wa chakula kwa kaya. Kaya zingine zina uwezo wa
kununua madawa ya kuulia wadudu, lakini madawa haya yana gharama kubwa
na yaweza kuwa na madhara kwa afya zao, (na kama yakiwa yameharibika
huwa hayafai kwa matumizi).
Mradi huu umebuniwa kutafiti ubunifu kwa ajili ya wakulima kuhusu matumizi ya
madawa asilia ya “diatomaceous earths” (vumbivumbi linalotokana na masalia ya
zamani ya viumbe wa majini), katika kuhifadhi mazao kama njia mbadala vijijini. Kwa
njia hiyo watafiti watawajibika kwanza kufanya majaribio na kulinganisha uwezo wa
madawa mbalimbali katika zoezi zima la kudhibiti wadudu waharibifu wa nafaka,
ziwapo ghalani. Awali, majaribio haya linganifu yatafanywa kwa kipindi cha miezi 8
kuendana na msimu wa kuhifadhi mazao, kuanzia Julai 2002 hadi Machi 2003.