Kwa ufupi:
Katika miaka ya karibuni, uendelezaji wa biofueli umekuwa ni agenda ya kawaida
duniani kote. Fueli zimiminikazo ambazo zinatokana na tungamotaka zinathibitisha
kuwa mbadala wa fueli za fosili hususani bidhaa za petroli katika hali ya mafuta ya petroli
na dizeli. Hivyo, biofueli zinaweza kutumika katika kupikia, kutoa mwanga, kuzalisha
umeme na kuendeshea vyombo vya usafiri. Biofueli kwa ufafanuzi ni fueli zitokanazo
na tungamotaka na zinaweza kuwa katika hali ya yabisi, gesi na kimiminika. Biofueli
yabisi ni pamoja na mkaa na kuni; biofueli gesi ni biogesi, gesi inayozalishwa katika
madampo yaliyofukiwa na udongo, n.k, na biofueli kimiminika inajumuisha mafuta
yanayotokana na mbegu za mimea au mimea yenyewe kama, ethano na biodizeli.