Kwa ufupi:
Mwongozo huu wa upitishaji wa Sheria Ndogo katika ngazi ya Kijiji umetokana na Sheria
za Serikali za Mitaa Mamlaka za Wilaya Sura 287 toleo la 2002 pamoja na Sera ya
Serikali ya kugatua madaraka kwa kukabidhi kazi, haki, wajibu pamoja na rasilimali fedha
kwa wananchi kupitia Serikali za Mitaa.
Aidha, changamoto mbalimbali zilizoko vijijini kupitia program mbalimbali kama vile
Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari, Mfuko ya Maendeleo ya Jamii
(TASAF), hifadhi ya Mazingira na Kilimo kwanza, zimetoa msukumo mkubwa kuwa na
haja ya kuwa na mwongozo kama huu unaowezesha vijiji kuandaa sheria zake ndogo
zitakazosaidia kukabiliana na changamoto hizo mfano kuhimiza watu kushiriki na
kuchangia kwenye shughuli za maendeleo na kushiriki kwenye ulinzi shirikishi katika
maeneo yao.