Kwa ufupi:
Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu millioni 20 nchini Tanzania hususan kutoka katika jamii zinazozunguka raslimali za misitu hutegemea Mazao si Timbao kwa ajili ya kuboresha hali ya maisha yao na kipato kazi. Licha ya utegemezi huo, haijulikani bado ni kwa kiasi gani Mazao si Timbao na jamii zinazotegemea mazao hayo zimeathiriwa na kutishiwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi; likiwemo suala zima la jinsi ya kukabiliana na athari hizo. Programmu ya Kujenga Uwezo wa Kudhibiti na Kukabiliana na Athari za Mabadiliko Hali ya hewa na Tabianchi, Tanzania (au CCIAM kwa lugha ya Kiingereza) unafadhili Mradi ujulikanao kama Mazao si Timbao na Ubora wa Maisha ya Jamii zinazoishi Kutegemea Raslimali za Misitu: Athari, Tishio na Ukabilianaji wa Mabadiliko Hali ya hewa na Tabianchi, Wilaya za Kilolo na Kilombero, Tanzania.
Mradi huu wa miaka mitatu (2011 – 2013) unalenga kujenga uwezo wa Taifa na wananchi kuelewa chanzo, tishio na athari za mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi na kuwapa mbinu za kukabiliana na athari za mabadiliko hayo katika kaya na jamii nzima kwa ujumla. Hii itasaidia kupunguza uharibifu wa raslimali za misitu, umasikini katika kaya na jamii nzima kwa kuwa na mbinu sahihi za kukabiliana na changamoto za mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi ndani ya mfumo mzima wa matumizi endelevu ya Mazao si Timbao, ambayo ni moja ya huduma muhimu zinazotolewa na raslimali za misitu. Inategemewa kwamba mwisho wa Mradi huu taarifa muhimu kuwasaidia wadau mbalimbali wakiwemo
watunga sera na sheria za kukabiliana na athari za mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi Tanzania. Mradi huu pia utachangia katika jitihada za serikali kupitia Mkakati wa Kupunguza Hewa Ukaa na uharibifu wa Misitu yaani MKUHUMI huku ukihakikisha uendelevu wa kipato kazi kwa jamii na usimamizi endelevu wa raslimali za misitu.
Mwongozo huu wa Kilimo cha Uyoga kukabiliana na mabadiliko hali ya hewa na tabianchi ni moja ya matokeo ya utafiti wa Mradi kwa kushirikiana na jamii zinazoishi kuzunguka Msitu wa Hifadhi wa New Dabaga-Ulongambi, Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa katika kutafuta mojawapo ya Mazao si Timbao ambayo ni muhimu katika jitihada za awali za kukabiliana na athari za Mabadiliko hali ya hewa na tabianchi. Utafiti wa Mradi umekwisha bainisha na jamii kukubali kuwa kuna mabadiliko hali ya hewa na tabianchi katika eneo hilo ambayo yanaleta athari na tishio kwa jamii hizo na Mazao si Timbao. Katika utafiti wa Mradi, zao la Uyoga unaokusanywa toka msituni lilipewa kipaumbele kama kati ya Mazao si Timbao manne yaliyo katika kipaumbele katika mikakati ya kukabiliana na athari
za mabadiliko hali ya hewa na tabianchi. Hata hivyo, katika maeneo ya Msitu wa Hifadhi wa New Dabaga-Ulongambi, Uyoga unaonekana kuanza kuadimika kutokana na athari za mabadiliko hayo ambayo yamebadili msimu wa upatikanaji na hata kupunguza kiasi cha uyonga mabo ungeweza kukusanywa na kutumiwa kikamilifu na jamii husika. Kuotokana na hayo, mbinu za kuotesha zao la Uyoga karibu na jamii lilijitokeza. Zao hilo la Uyoga lilionekana linaweza kuisaidia jamii kujipatia chakula na kipato na hivyo kuweza kusaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko hali ya hewa na tabianchi lakini jamii haikuwa na utaalamu au teknolojia rahisi ya jinsi ya kuuotesha nje ya mazingira ya misitu. Kutokana na hali hiyo, Mradi uliona ni vema kuandaa Mwongozo utakaosaidia kutoa mafunzo kwa jamii juu ya Kilimo bora cha Uyoga kama njia mojawapo ya kukabiliana na
athrai zinazoletwa na Mabadiliko hali ya hewa na Tabianchi. Mwongozo huu umeandaliwa kwa kupitia majarida na machapisho mbalimbali ya kiutafiti na hivyo unaweza kutumika hata katika maeneo mengine ya Tanzania na sehemu nyingine ili kuinufaisha jamii husika.