Ghala la Mkulima

MICHAKATO YA KUHIFADHI VYAKULA MBALIMBALI KWA KUKAUSHA.

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Denis, Marco,D.
dc.date.accessioned 2022-01-25T10:53:30Z
dc.date.available 2022-01-25T10:53:30Z
dc.date.issued 2017-05-12
dc.identifier.citation MICHAKATO YA KUHIFADHI VYAKULA MBALIMBALI KWA KUKAUSHA.Wakulima wengi huingia hasara kubwa pale mazao yao yanapoharibika kwa kukosa masoko. Kufahamu michakato ya ukaushaji mazao utawawezesha kuyaweka katika hali ya kutoharibika na hivyo kuweza kutumiwa kwa muda mrefu. Pia ukaushaji huwezesha vyakula kutumika kwa muda mrefu bila kuharibu ladha na ubora wake.Ukaushaji wa vyakula mbalimbali hutumiwa na wakulima wengi kama njia mojawapo ya kuepusha uharibifu wa mazao na kuviwezesha kutumika kwa muda mrefu. Yafuatayo ni maelezo ya michakato mbalimbali inayotumika kuvikausha vyakula hivyo.MBOGA: Majani ya kunde, Matembele, Mchicha na Majani ya Maboga.* Chambua mboga vizuri na chuma majani machanga.* Safisha mboga vizuri* Chemsha kwenye maji ya moto kwa dakika 1-5 (inategemeana na ugumu wa mboga, laini ni dakika chache na ngumu ni dakika nyingi) kwenye maji yenye chumvi ili rangi ya kijani iaitoke.* Chuja kwa kutumia chekeche* Anika nje kwenye chombo safi kama mkeka, ungo, chekeche. Epuka kukausha kwenye jua kali, anika kivulini na jua la asubuhi kabla halijawa kali.* Kausha mpaka mjani yavunjike kwa urahisi na geuza geuza mara kwa mara.* Weka katika chombo kinacho funika kama debe, kopo n.k.MATUNDA: Nyanya, Ndizi, Maembe, Tende, Zabibu, Ukwaju, Nanasi.* Tumia kisu kisichopata kutu kwa kukata matunda ili kuzuia matunda kuwa meusi.* Osha na katakata vipande vyembamba. Ndizi ni lazima umenye.* Tende, zabibu, ukwaju unaanika hivyo hivyo nzimanzima.* Ndizi chemsha kwa dakika 5 katika maji ya chumvi ili kuzuia rangi mbaya isitokee.* Kausha taratibu kwenye jua la kiasi mpaka zikauke.* Weka katika vyombo visivyoingiza unyevu.Kabeji* Osha na katakata vipande vyembamba* Chemsha kwa dakika 2 tu kwenye maji yenye chumvi.* Chuja na anika kwebye chombo safi mpaka zikauke.* Weka katika vyombo visivyoingiza unyevu.Kisamvu* Angalia majani laini na twanga.* Chemsha katika maji yenye chumvi kidogo kwa dakika kumi ili kupunguza sumu hasa kama umechuma majani ya muhogo.* Kausha katika chanja kwa kutumia mkeka safi, ungo au chekeche.* Weka katika chombo kisichoingiza unyevu.MIZIZI: Viazi vitamu na mihogo.* Tumia viazi au mihogo iliyokomaa.* Menya, katakata vipande vyembamba kidogo.* Safiasha au chemsha katika maji kwa dakika tano.* Kausha katika chanja na katika hali ya usafi.* Ikikauka weka kwenye chombo safi kisichoingiza unyevu.Imetayarishwa na Marcodenis E. Misungwi, mtaalam wa kilimo na mif en_US
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123456789/565
dc.description Kuhifadhi Vyakula en_US
dc.description.abstract Wakulima wengi huingia hasara kubwa pale mazao yao yanapoharibika kwa kukosa masoko. Kufahamu michakato ya ukaushaji mazao utawawezesha kuyaweka katika hali ya kutoharibika na hivyo kuweza kutumiwa kwa muda mrefu. Pia ukaushaji huwezesha vyakula kutumika kwa muda mrefu bila kuharibu ladha na ubora wake. Ukaushaji wa vyakula mbalimbali hutumiwa na wakulima wengi kama njia mojawapo ya kuepusha uharibifu wa mazao na kuviwezesha kutumika kwa muda mrefu. Yafuatayo ni maelezo ya michakato mbalimbali inayotumika kuvikausha vyakula hivyo. en_US
dc.description.sponsorship Muungwana Blog. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Kilimo foram en_US
dc.subject MICHAKATO YA KUHIFADHI VYAKULA MBALIMBALI KWA KUKAUSHA. en_US
dc.title MICHAKATO YA KUHIFADHI VYAKULA MBALIMBALI KWA KUKAUSHA. en_US
dc.type Other en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu