Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya
Kilimo na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo,
kinatekeleza mradi wa Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya
kwa Wakulima Wadogowadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza
rasmi Septemba 2000, unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia
Shirika lake la Maendeleo (NORAD).
Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya
mradi na pia kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na
., washauri wa wakulima ni kufanya warsha zenye madhumuni
yafuatayo:
1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili
kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji
kushirikishwa pande zote kwa lengo la kufanikisha kilimo
2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili
wakulima wadogowadogo
3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au
kipaumbele zaidi
4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya
kilimo.
Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya
Wakulima waKanda ya Mashariki Kuhusu Matatizo ya Masoko ya
Mazao ya Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa VETA, Tanga,
tarehe 24-26 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na
kutolewa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.