Kwa ufupi:
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo
na Chakula, na Chuo Kikuu cha Norway cha Kilimo, kinatekeleza mradi wa
Utafiti wa Uhakika wa Chakula na Pato la Kaya kwa Wakulima Wadogo
wadogo Tanzania. Mradi huu ambao ulianza rasmi mwezi Septemba 2000,
unagharamiwa na Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo
(NORAD).
Kati ya shughuli muhimu zilizopangwa ili kutekeleza malengo ya mradi na
kuimarisha uhusiano wa wakulima, watafiti na washauri wa wakulima ni
kufanya warsha zenye madhumuni yafuatayo:
1. Kuwajumuisha watafiti, wakulima na washauri wa kilimo ili
kudadisi kuhusu mambo muhimu yanayohitaji ushirikishwaji wa
wadau wote kwa lengo la kufanikisha kilimo
2. Kuchambua na kuainisha matatizo yanayowakabili wakulima
wadogo wadogo
3. Kupanga ili kutambua mambo gani yapewe uzito au kipaumbele
zaidi
4. Kushiriki katika kupeana uzoefu wa maeneo muhimu ya kilimo.
Chapisho hili linawasilisha mwenendo wa Warsha ya Nne ya Wakulima wa
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Kuhusu Matatizo ya Masoko ya Mazao ya
Wakulima, iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Anglikana, Iringa,
tare he 6-8 Juni 2002. Mwenendo wa warsha umechapishwa na kutolewa
katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.