Ghala la Mkulima

Unafuu wa mbolea za ruzuku.

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.contributor.author Mamalaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania
dc.date.accessioned 2024-09-02T10:24:43Z
dc.date.available 2024-09-02T10:24:43Z
dc.date.issued 2023-09
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/910
dc.description Jarida en_US
dc.description.abstract Katika harakati za kuimarisha kilimo, serikali ya Tanzania mwaka jana ilitenga shilingi bilioni 150 kama ruzuku ya mbolea kwa wakulima kuwasaidia waongeze uzalishaji na kupunguza makali ya bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia, hasa baada ya kuzuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine. Kwa mujibu wa Dkt. Ngailo, katika siku za usoni Tanzania itakuwa kitovu cha mbolea barani Afrika kama mikakati ya sasa iliyobuniwa na serikali ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya mbolea itakwenda kama ilivyopangwa. Hivi sasa Tanzania inashuhudia kasi ya ujenzi wa viwanda vya mbolea ili kukidhi mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika sekta ya kilimo. Nia ya kasi ya ujenzi wa viwanda vya mbolea ni kuwapunguzia wakulima bei ili mbolea ipatikane kwa urahisi kwa kuwafikia wakulima hao mahali walipo. Lengo jingine la kuwavuta wawekezaji katika ujenzi wa viwanda ni kuwa na soko linaloaminika la bidhaa hiyo kwa nchi jirani za Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika pamoja na mataifa mengine ya Ulaya ambayo yamekuwa yakiiagiza mbolea kutoka kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara. Mahitaiji ya mbolea kwa wakulima wa Tanzania katika miaka ya karibuni yameongezeka kutoka tani 42,000 mpaka tani165,000 baada ya kuwepo kwa jitihada za kuwaelimisha wakulima kutumia mbolea ili waongeze tija katika mashamba yao, kwamujibu wa Bole. Ni faraja kwamba ongezeko la matumizi ya mbolea limezaa matunda baada ya kushuhudia ongezeko la uzalishaji wa chakula kutoka tani milioni 17 hadi kufikia tani milioni 20, anaeleza Dkt. Ngailo. “Kazi ya kuwaelimisha wakulima kutumia mbolea ni suala endelevu kwa kushirikiana na serikali za mitaa. Kuna uwezekano mkubwa kwa wakulima wengi Tanzania kutumia mbolea na hatimaye kulilisha bara la Afrika,” anaeleza Dkt. Ngailo. “Ruzuku ya mbolea imesaidia sana wakulima kununua mbolea kwa wingi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.’ Dkt. Ngailo anaeleza kuwa ongezeko la matumizi ya mbolea miongoni mwa wakulima limewapa viongozi ari ya kujiamini kwamba Tanzania katika miaka michache ijayo itafikia lengo lake la kulisha bara zima la Afrika kutokana na ziada ya chakula kinachozalishwa. “Inawezekana kwa Tanzania kulisha Afrika na dunia nzima. Tuna uwezo wa kuzalisha chakula cha ziada kukidhi mahitaji ya Afrika na dunia nzima,” anasema kwa kujiamini , huku akiungwa mkono na mchumi mwandamizi wa TFRA, Elizabethi Bole. Kwa dhamira ya Tanzania kujitosheleza kwa chakula na kuwa ghala la kuaminika kwa Afrika na dunia nzima, mkutano wa 13 wa Jukwaa la Chakula Afrika 2023 utakuwa na mambo mengi ya kujionea ambayo yatafaa yaigwe na mataifa mengine kuwa fundisho. Kama alivyosema Dkt. Stephan Ngailo, dunia itakuja Tanzania kushuhudia yaliyopo na itaondoka na mafunzo kwenda kuyapandikiza sehemu nyingine; na hivyo kuliuza jina la Tanzania ughaibuni. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania en_US
dc.relation.ispartofseries ;toleo namba:19
dc.subject Mbolea en_US
dc.subject Mbolea ya Ruzuku en_US
dc.title Unafuu wa mbolea za ruzuku. en_US
dc.title.alternative :Rais Samia ataka unafuu mbolea ya ruzuku en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu