Ghala la Mkulima

Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna. Kitabu na. 1

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

dc.date.accessioned 2018-01-04T10:53:03Z
dc.date.available 2018-01-04T10:53:03Z
dc.date.issued 2003
dc.identifier.isbn 9987 - 400 - 04 - 3
dc.identifier.uri http://10.10.11.5/handle/123/79
dc.description.abstract Nafaka ni mazao makuu ya chakula ambayo hutumiwa na watanzania wote waishio mijini na vijijini. Nafaka zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu kuliko mazao mengine ya chakula na mara nyingi nafaka huzalishwa mara moja au mbili kwa mwaka. Kwa hiyo ili iweze kupatikana na kutumika kwa wakati wote ni lazima kuhifadhi. Aidha ili kuweza kuwa na bidhaa zenye thamani ni lazima kusindika. Jitihada zimekuwa zikifanywa na seikali kuongeza tija na uzalishaji wa mazao hayo. Uzalishaji wa mazao ya nafaka unakadiriwa kufikia wastani wa tani 3, 897,500 kwa mwaka. Pamoja na ongezeko la uzalishaji, teknolojia zinazotumika katika uvunaji, utayarishaji na hifadhi ni duni na husababisha upotevu mkubwa wa mazao hayo. Wastani wa tani 1,559,000 za mazao ya nafaka hupotea kila mwaka. Aidha upotevu mkubwa hutokea katika maghala kutokana na kuhifadhi nafaka ambayo haijakauka sawasawa na pia kutokana na mashambulizi ya wadudu waharibifu. Kuongeza uzalishaji pekee hakutakuwa na maana ikiwa juhudi za makusudi hazitachukuliwa kupambana na matatizo yasababishayo upotevu wa mazao hayo. Teknolojia sahihi za utayarishaji wa mazao kabla ya kuhifadhi zisipotumika, nafaka itaharibika hata kama ingehifadhiwa katika ghala bora. Hivyo ni vyema kutumia njia bora za kutayarisha nafaka kama vile kukausha vyema, kusafisha na kufungasha ili kupunguza uharibifu unaosababisha upotevu wa mazao. Lengo la uandaaji wa kitabu hiki ni kuelimisha jamii kuhusu teknolojia sahihi za uvunaji, utayarishaji, ufungashaji, usindikaji na hifadhi ya mazao ya nafaka baada ya kuvuna. Aidha matumizi bora yanayokidhi mahitaji ya lishe ya mazao hayo yameainishwaili kupunguza tatizo la utapia mlo na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na kuongeza kipato. Walengwa wa kitabu hiki ni wakulima na wadau wengine ambao wamejiajiri katika sekta ya kilimo. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Wizara ya Kilimo na Chakula, Idara ya usalama wa chakula. en_US
dc.subject Chakula en_US
dc.subject Hifadhi en_US
dc.subject Mazao en_US
dc.subject Kilimo en_US
dc.subject Nafaka en_US
dc.subject Kuvuna en_US
dc.subject Usindikaji en_US
dc.title Teknolojia za Utayarishaji, Usindikaji na Hifadhi ya Mazao ya Nafaka baada ya Kuvuna. Kitabu na. 1 en_US
dc.type Book en_US


Files in this item

kinaonekana kwenye vifungu vifuatavyo

xmlui.ArtifactBrowser.ItemViewer.show_simple

Tafuta kwenye mkulima


Peruzi

My Account

Takwimu