Kwa ufupi:
Zao la dengu ni moja ya mazao muhimu katika kuinua pato la mkulima nchini Tanzania,
hivyo katika msimu wa202012021, Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) kwa kushirikiana na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) pamoja na uongoziwa mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Manyara na halmashauri zake husika zitasimamia uendeshaji wa minada ya dengu katika ghala zinazotumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala. Mauzo hayo yanalenga kuleta bei zenye ushindani wa haki, uwazi na kupunguza gharama za ununuziwa zao la dengu.