Kwa ufupi:
MWONGOZO HUU UMEANDALIWA ILI KUWEZESHA KUWAFUNDISHA wakulima katika ukuzaji wa biashara, hivyo kuwezesha wakulima wanaofanya kilimo cha kujikimu kubadilisha kutoka kulima kwa ajili ya chakula cha familia tu hadi kilimo kama shughuli ya kibiashara. Mwongozo huu una lengo la kuwapa wakulima ujuzi, mtazamo, na ustadi unaohitajika kubadilisha na kukuza biashara zao kwa namna endelevu ili ziwe biashara za kilimo zenye mafanikio. Mwongozo huu unaangazia dhana za msingi kuhusu uwekezaji, kanuni za msingi kuhusu mnyororo wa thamani, huduma muhimu za ukuzaji wa biashara, namna ya kutumia soko kwa mafanikio, usimamizi wa fedha na ujuzi wa upangaji wa biashara ulio muhimu katika kufanikiwa kwa mjasiriamali anayejihusisha na kilimo biashara.