Kwa ufupi:
Bodi ya Utoaji wa Leseni za Ghala Tanzania ni wakala ya serikali chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda. Wakala hii ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Stakabadhi Ghalani Namba 10 ya mwaka 2005. Dhamira ya Bodi ni kusimamia na kuhimiza Mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaohakikisha upataji endelevu na usio na upendeleo wa mifumo rasmi ya mikopo na uuzaji wa bidhaa, na inatarajiwa kutimizwa kwa kutekeleza kazi zake za utoaji wa leseni za biashara ya ghala, waendesha na wakaguzi wa maghala kwa kusimamia mfumo wa jumla. Katika kufanya hivyo, Bodi inakusudia kufikia dira yake ya kuwa shirika linaloongoza katika kuwaunganisha wazalishaji wa bidhaa kwenye utafutaji mikopo rasmi kwa kutumia njia yenye tija na yenye ufanisi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani.
Tangu Bodi hii ilipoanzishwa, imeendelea kutekeleza kazi zake kwa kutumia muundo wa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Stakabadhi Ghalani, Kanuni za Ghala, Mwongozo wa Uendeshaji na miongozo elekezi ya mara kwa mara.
Ni maoni yangu kwamba, kwa kuwa na uendeshaji wenye tija na ufanisi wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, mwongozo huu utawasaidia watendaji wakuu kupata uelewa wa jumla, maarifa, uzingatiaji wa taratibu, majukumu yao na haki katika kuendesha mfumo huu.
Umetayarishwa kutokana na uzoefu, changamoto na mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chote cha uendeshaji wa mfumo kwa mazao mbalimbali na maeneo ya kijiografia nchini Tanzania.