Kwa ufupi:
Mihogo asili yake ni tropiki ya Amerika ya Kusini. Ililetwa katika bonde la Congo katikati mwa
miaka ya 1500, na Afrika Mashariki miaka ya 1700. Asilimia 93 ya mihogo inayozalishwa
hutumika kama chakula, hii kulifanya zao la muhogo kuwa muhimu kwa ajili ya usalama wa
chakula vijijini. Zaidi ya watu milioni 500 kusini mwa jangwa la Sahara hutegemea mihogo kama
chakula kikuu.
Tanzania ni nchi ya nne inayozalisha mihogo kwa wingi Afrika. Inazalisha takribani tani milioni
saba kwa mwaka katika maeneo mengi nchini. Asiliia 84 ya mihogo hii hutumika kama chakula cha
binadamu.