Kwa ufupi:
Hifadhi bora ya mazao inahakikisha familia inakuwa na chakula
cha kutosheleza mwaka mzima. Pia mazao yanaweza kuuzwa
wakati wowote ili kuongeza kipato. Mradi wa hifadhi bora ya
mazao na udhibiti wa viumbe waharibifu umebuniwa na watafiti
wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA),na unafadhiliwa
na Programu ya FOCAL,SUA. Mradi huu unawalenga wakulima
katika wilaya tatu Tanzania ambazo ni Handeni, Mvomero na
Iringa Vijijini.
Hifadhi bora na udhibiti wa wadudu, panya na viumbe wengine
wanaoharibu mazao ghalani ni muhimu ili kuhakikisha mazao
kama mahindi, kunde, maharage, mpunga, n.k. yanayozalishwa
na wakulima hayaharibiwi wakati yanapohifadhiwa. Utafiti
shirikishi unafanyika juu ya mbinu za asili na za kisasa ili
kuboresha hifadhi ya mazao na kudhibiti viumbe waharibifu wa
mazao ghalani.